Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Hassan Khalil, Naibu wa Kisiasa wa Bunge la Lebanon, akiwa na kamanda Amirian, Mkurugenzi wa Makumbusho, alitembelea mandhari ya muqawama ya Shahidi Haj Qasem Soleimani.
Katika ziara hiyo, Hassan Khalil alijifunza kuhusu sehemu mbalimbali za simulizi za muqawama katika eneo hilo na aliona kwa karibu jinsi mapambano ya mataifa ya eneo yanavyooneshwa, pamoja na mchango mkubwa wa Shahidi Soleimani.
Ali Hassan Khalil alishukuru juhudi za makumbusho na kusema: “Nilichokiona katika mandhari hii ni picha sahihi na ya kuhamasisha ya muqawama wa mataifa ya eneo. Mandhari hii inaonesha jinsi fikra na vitendo vya Shahidi Haj Qasem Soleimani vilivyoleta roho mpya katika mhimili wa muqawama.”
Aliongeza kuwa; simulizi hizi ni za thamani kubwa kwa vizazi vijavyo, kwa sababu zinawasilisha ukweli wa kusimama dhidi ya dhulma na uvamizi kwa njia iliyo wazi na yenye ushahidi.
Naibu huyo pia alisisitiza kuwa: “Watu wa Lebanon daima wanajiona kuwa upande mmoja na watu wa Iran na pamoja na mhimili wa muqawama. Ushirikiano huu una mizizi katika imani na malengo ya pamoja.”
Inafaa kuashiriwa kuwa mandhari ya muqawama ya Shahidi Soleimani, ambayo ni sehemu muhimu ya Makumbusho ya Kitaifa ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na Vita vya Kujihami, imeundwa kwa msingi wa simulizi ya upinzani dhidi ya mfumo wa kiutawala na kwa mujibu wa fikra za Mapinduzi ya Kiislamu.
Mandhari hii inaendelea na historia ya Mapinduzi ya Kiislamu na vita vya miaka minane vya kujihami, ikisimulia harakati za muqawama duniani kote, na inalenga kuwasilisha picha halisi, yenye ushahidi na ya kuhamasisha kuhusu juhudi za mataifa ya eneo.
Maoni yako